Rais Uhuru ahandwa aokoe Ligi Kuu Kenya

Muktasari:

Baada ya kupachika Rais alionekana kufurahia bao hilo na sasa Omondi katumia fursa hiyo kumhanda kuhusu masuala ya soka nchini.

Nairobi, Kenya.WINGA wa Gor Mahia, Boniface Omondi aliyepachika bao pekee na la ushindi kwenye makala ya 89 ya Mashemeji Derby juzi Jumapili, sasa kamrai Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kuokoa Ligi ya KPl inayotishia kuangamia.

Omondi katoa ombi lake baada ya kupachika bao mbele ya Rais Uhuru ambaye aliwashangaza wengi kwa kufika uwanjani kuhudhuria mechi yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa rais.

Wing’a huyo alipachika bao hilo dakika ya 27 kutokana na mpira wa kona uliwashinda mabeki wa AFC Leopards kuuthibiti na kumruhusu ausukume wavuni kiulaini wenzake wakiwa wamezubaa.

Baada ya kupachika Rais alionekana kufurahia bao hilo na sasa Omondi katumia fursa hiyo kumhanda kuhusu masuala ya soka nchini.

Omondi kamtumia Rais salamu akimwomba aiokoe soka la Kenya hasa ligi ambayo imesota vibaya sana tangu Kampuni ya Sportepsa aliyoikazia maisha kiongozi huyo, kusitisha udhamini na kisha kujiondoa kwenye soko la nchini.

“Ni matumaini yangu Rais ataendelea kutenga muda zaidi wa kuja uwanjani kushuhudia mechi hizi sababu kando na kupata burudani, itatoa fursa kwake kuweza kuelewa baadhi ya changamoto zinazoikumba soka letu. Ombi langu kwake kwa sasa ni kumrai tu aone ni jinsi gani ligi inaweza ikapata fedha za kutoshwa kuendeshwa sababu wachezaji wengi huu mpira ndio tunategemea kulisha familia zetu. Sasa hivi mambo ni magumu sana timu zinahangaika, wachezaji tun aumia sababu hakuna hela,” Omondi karai.