Rado apata 'dili' la maana

Monday October 1 2018

 

By Rhobi Chacha

 Dar es Salaam. Mwigizaji wa filamu nchini, Simon Mwapagata 'Rado' amepata 'dili' la kuteuliwa kuwa balozi wa kinywaji cha Zhimwa Portable Spirit kinachotengenezwa na  Kampuni ya Canon  General Supplier.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho leo Jumatatu ya  Oktoba Mosi, Rado ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kwa mshahara wa millioni mbili kwa mwezi amesema.

 "Napenda kuishukuru Kampuni ya Canon General Supplier kwa kunichagua kuwa balozi wao wa Zhimwa Portable Spirit. Nimeipokea kwa mikono miwili na naahidi kuwa balozi mzuri naomba kuungwa mkono,"alisema Rado.

Amesema wasanii wanapochaguliwa kuwa mabalozi ni njia mojawapo ya kujitangaza wao na kazi  wanazofanya, ameziomba kampuni nyingine pia zijitangaze kupitia sanaa.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa Kampuni Canon  General Supplier amesema, wamemchagua Rado kwa sababu ni msanii mwenye kipaji cha pekee hivyo basi atawasaidia kukitangaza kinywaji hicho ambacho ni kipya sokoni.

Advertisement