Prisons wanasajili kimya kimya

Muktasari:

  • Uongozi wa Prisons umeamua kufanya usajili wao kimya kimya kwa madai wanahitaji kufanya mambo kwa umakini ndipo wayalete kwa jamii.

PRISONS wameanza mchakato wa usajili lakini usajili huo unafanya kimya kimya kwa madai kuwa wanachunguza kwanza mikataba ya wachezaji wanaowahitaji.
Katibu Mkuu wa Prisons, Ajabu Kifukwe amesema wanahitaji kuwa makini kwenye usajili ili kukwepa kesi za mikataba zinazopelekwa Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Alisema wanafanya hivyo kwasababu baadhi ya wachezaji sio wakweli kuhusu mikataba yao na timu wanazotoka, hivyo hawataki kushitakiwa.
"Hakuna kipindi kigumu kama usajili na kila timu ina utaratibu wake, Prisons hatutaki kutangaza mchezaji  ambaye hatuna uhakika naye kama tutamsajili au la.
"Ndio maana tunaamua kufanya mambo kimya kimya, ikifikia hatua tumemalizana na mchezaji ndipo tunamuweka wazi, lengo ni kuwa mfano kwa jamii kwa kile ambacho tunakifanya"anasema.
Anasema nafasi ambazo wanataka kusajili ni beki wa kati, kiungo, mshambuliaji na kipa.

xxxxxx