Prisons mchana kweupe, Kimenya akatema cheche!

Muktasari:

  • Kikosi cha Tanzania Prisons kimefanya maandalizi ya mchezo wao na Singida United mchana wa jua kali lengo ni kwenda sawa na mazingira ya mechi na beki wao Salum Kimenya amesisitiza morali iko juu.

Dar es Salaam. Kikosi cha Tanzania Prisons kinapiga mazoezi mchana na jua kazi lakini kiraka wa kikosi hicho, Salum Kimenya amesema ndiyo kwanza mzuka umepanda na sasa ni kazi tu.
Kimenya ambaye amejiunga na Tanzania Prisons siku mbili zilizopita akitokea kwenye kambi ya Taifa Stars ambako walikuwa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON zitakazofanyika nchini Cameroon amesema.
"Licha ya kufanya mazoezi mchana kwenye jua kali watu wana morali ya juu kwa lengo la kuanza kwa kasi mechi za Ligi Kuu,"alisema Kimenya ambaye mbali na kucheza nafasi ya beki wa kulia, ana uwezo wa juu wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kama winga na kiungo.
Amesema, lengo la kikosi hicho kufanya mazoezi katika hali hiyo ni kujiandaa na mchezi wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Singida United utakaopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
"Tutacheza mchana saa nane, hivyo kocha akaona ni vizuri hata mazoezi yakafanyika katika muda huo huo,"alifafanua.
Akizungumzia uwepo wake Taifa Stars na namna ilivyobadirisha kiwango chake cha soka.
"Kucheza Taifa Stars ni hakua na heshima lakini mbali na yote hayo kuna mambo mengi ya kujifunza hapo,"alisema.