Wasiojulikana wamteka bosi wa Simba MO Dewji

Thursday October 11 2018

Dar es Salaam. Taarifa zilizotufikia mpaka sasa ni kwamba Mfanyabiashara maarufu Mohamed Dewji MO anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana.
Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo wakati Mo  akifika katika Hoteli ya Colloseum kwa ajili ya kufanya mazoezi.
Taarifa kutoka hapa hotelini kwamba walimteka walifika mapema hotelini hapo kisha alipofika Mo wakamchukua na kupiga risasi juu na kuondoka naye.
Tayari eneo la tukio viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mliro, Msemaji wa Simba, Haji Manara wako hotelini hapo kujua kilichotokea.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, MO alikwenda akiendesha mwenyewe gari hakuwa na dereva  na dereva wake ndiyo amefika muda huu.
Wenyeji wa hoteli hii wanasema Mo amekuwa akifika mwenyewe asubuhi akiendesha gari yake na anapomaliza huondoka na kukutana na dereva wake huko kwake.

Advertisement