Pilato wawili Kenya kuamua AFCON

Muktasari:

 

 

  • Mwamuzi wa kati Peter Waweru, ambaye ni mhadhiri wa hesabu katika chuo kikuu cha Jomo Kenyatta pamoja na refa msaidizi Gilbert Cheruiyot wameteuliwa.

WAAMUZI Wakenya wawili wameteuliwa kusimamia mechi za fainali ya kombe la mataifa bora barani (AFCON) kule Misri kwanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Mwamuzi wa kati Peter Waweru, ambaye ni mhadhiri wa hesabu katika chuo kikuu cha Jomo Kenyatta pamoja na refa msaidizi Gilbert Cheruiyot wameteuliwa.

Jumla ya marefa wa kati kutoka nchi ishirini wametajwa kwenye orodha ya mwanzo kabisa na Shirikisho la Soka barani (CAF).

Waweru hajawahi kusimamia mechi za fainali kwenye AFCON na hii itakuwa mara yake ya kwanza japo amesimamia za kufuzu sawia na fainali za chipukizi wasiozidi umri wa miaka ishirini kule Niger mwezi Februari.

Marefa tajika kutoka Kenya kama Davies Omweno wametemwa nje.