Peter Tinno aipa ujanja Stars Cape Verde

Muktasari:

Msafara wa Stars ambao uliondoka Jumatano saa 9 alfajiri kuelekea Praia, Cape Verde pia yupo Tino ambaye alifunga bao lililoiwezesha Stars kushiriki kwa mara ya kwanza na ya mwisho kwenye fainali za AFCON mwak 1980.

Tino ni miongoni mwa nyota wenye historia ya kipekee kwenye timu ya Taifa akiwa ndiye aliyeivusha kushiriki kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 1980 ambazo zilikuwa za mwisho kwa Tanzania kushiriki.
Kujumuishwa kwa Tino kunaonekana kunalenga kuongeza hamasa na molali kwa wachezaji wa Stars kushinda mchezo huo dhidi ya Cape Verde ili ijiweke katika mazingira mazuri ya kufuzu AFCON mwakani.
Stars inashika nafasi ya tatu kwenye kundi L ikiwa na pointi mbili nyuma ya Uganda yenye pointi nne na Lesotho yenye pointi mbili huku Cape Verde ikishika mkia ikiwa na pointi moja.