Pesa noma Charles Baba, Kalala Junior watekwa Simba

Wednesday August 8 2018

 

By Doris Maliyaga

Dar es Salaam. Pesa noma sana, kwani waimbaji wa Twanga Pepeta, Kalala Junior na Charles Baba imewabidi waishabikie Simba bila kupenda wakati wao ni Yanga wa kulia.

Waimbaji hao ambao wanajulikana kuwa ni wanazi wa Yanga  wemetamka wazi wakati wa tamasha la Simba

Day kuwa pesa ndiyo sababu wako hapo.

Wakiwa wamevalia jezi za sare ya Simba ambazo nyuma zimechapishwa majina yao.

Wamesema, walifanya maamuzi hayo jana Jumanne na leo Jumatano wakaingia uwanjani kwa staili hiyo.

"Ebwana mpango wa pesa dada si unajua. Jana tu ndiyo tulichukua maamuzi haya,"alisema Charles Baba.

Waimbaji hao maarufu katika miondoko  ya bolingo, waliabatana na bendi ya Twanga Pepeta na kutumbuiza katika sherehe hizo.

Advertisement