Pep anapiga sala kisa mastaa wake

Muktasari:

Guardiola kwa sasa ana majeruhi watano kwenye kikosi chake huku kwenye mechi hizo za kimataifa wachezaji wake 14 watakwenda kuungana na timu zao za taifa. Anachoamini ni kwamba kutimiza ndoto za kubeba mataji manne basi anahitaji kuwa na wachezaji wake wote wakiwa fiti kwenye kikosi hasa baada ya mapumziko ya siku 10 ya mechi za kimataifa.

MANCHESTER, ENGLAND.PEP Guardiola atakuwa na kazi moja tu muhimu ya kupiga sala ili wachezaji wake warudi bila ya majeruhi watakapokuwa kwenye michezo ya kimataifa.

Kocha huyo Mhispaniola, Guardiola analazimika kuomba sana wachezaji wake wasiumie baada ya kukabiliwa na ratiba ngumu kwelikweli kwa mwezi ujao wa Aprili.

Kikosi cha kocha huyo Manchester City kitakuwa na shughuli ya mechi 14 ndani ya wiki saba kuanzia mwishoni mwa mwezi huu, hasa baada ya kuendelea kuwapo kwenye mikikimikiki ya makombe mengine.

Guardiola kwa sasa ana majeruhi watano kwenye kikosi chake huku kwenye mechi hizo za kimataifa wachezaji wake 14 watakwenda kuungana na timu zao za taifa. Anachoamini ni kwamba kutimiza ndoto za kubeba mataji manne basi anahitaji kuwa na wachezaji wake wote wakiwa fiti kwenye kikosi hasa baada ya mapumziko ya siku 10 ya mechi za kimataifa.

Guardiola alisema: “Kuomba dua ni kitu anachokifanya. Naomba wachezaji wangu warudi wakiwa fiti. Nataka iwe hivyo.”

kitendo cha kutinga nusu fainali ya Kombe la FA hiyo ina maana kwamba Man City itabidi ratiba yao ya Ligi Kuu England dhidi ya Cardiff City itabadilishwa. Mastaa Kevin De Bruyne, John Stones na Benjamin Mendy ni miongoni mwa wachezaji majeruhi, wakati Fernandinho hatakuwapo uwanjani kwa kipindi kirefu hata baada ya mechi za kimataifa kumalizika.