Pawasa awapeleka Chirwa, Chilunda Simba

Muktasari:

Pawasa alisema Chirwa ni kati ya wachezaji ambao wanaweza kufiti timu yoyote kwa hapa Afrika kutokana na aina yake ya uchezaji wa kupambana kwa kutumia nguvu na akili.


BEKI wa zamani mwenye heshima ndani ya Simba, Boniface Pawasa anadhani mastraika, Obrey Cirwa na Shabaan Chilunda wanafaa kuongezwa kwenye kikosi cha Sven Vandenbroeck msimu ujao.

Siyo huyo tu, kwenye ulinzi amemtaja beki Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union ya Tanga.

Pawasa alisema Chirwa ni kati ya wachezaji ambao wanaweza kufiti timu yoyote kwa hapa Afrika kutokana na aina yake ya uchezaji wa kupambana kwa kutumia nguvu na akili.

“Simba inaweza ikawatazama wachezaji kama Bakari Mwamnyeto, Novatus Kufunga, Cosmas yupo Biashara U-20, Shaban Chilunda(Azam) kwa mshambuliaji wakimpata Obrey Chirwa (Azam).

“Hao ni wachezaji baadhi tu kwani kama kunakuwa na watu maalumu kwa ajili ya kuwafuatilia basi wanaweza wakaboresha kikosi kikawa imara zaidi,” alisema mchezaji huyo msomi.

Mkongwe mwingine, Emmanuel Gabriel alisema; “Wasajili beki wa kati na mshambuluaji wa kulazimisha mashambulizi ambaye atakuwa anatumia akili nyingi za kuwasumbua wapinzani.”