Pauni 12 milioni kumtimua Mourinho Man United

Tuesday August 7 2018

 

London, England. Manchester United watalazimika kumlipa Jose Mourinho kiasi cha pauni12milioni kama wanataka kumfukuza Mreno huyo msimu huu.

Kocha huyo Man United ameweka wazi kuwa hana furaha baada ya kupata matokeo mabaya katika ziara yao ya Marekani.

Mourinho pia amekosa ushirikiano kama alivyotegemea katika usajili na sasa tumaini lake ni kupata mchezaji mmoja tu.

Mourinho amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa sasa anajua kuwa atapokea pauni12milioni kwa msimu kama atafukuzwa.

Lakini inafahamika kwamba atapokea mshahara wake wa miezi 12, baada kutokana na mkataba wake.

Mourinho yupo katika presha kubwa ya kuhakikisha anafanikiwa msimu huu, lakini anahisi kwamba hajapata kuungwa mkono vya kutosha katika dirisha la usajili.

Advertisement