Pambano la Joshua vs Andy Ruiz Jr wasichana wapigwa stop Saudi Arabia

Muktasari:

Katika pambano hilo litakalofanyika Jumamosi usiku kwa mara ya kwanza hakutakuwa na wale wasichana wanaopita kuonyesha raundi kila inapotaka kuanza.

Macca, Saudi Arabia. Hakutakuwa na msichana wa kuonyesha bango la kuanza kwa raundi wakati wa pambano la ngumi kati ya Anthony Joshua na Andy Ruiz Jr kwa sababu ya kuheshimu utamaduni wa Saudi Arabia.

Katika pambano hilo litakalofanyika Jumamosi usiku kwa mara ya kwanza hakutakuwa na wale wasichana wanaopita kuonyesha raundi kila inapotaka kuanza.

Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kuheshimu utamaduni wa Saudi Arabia, ambao sheria zao zinakataza wanawake kujitokeza hadharani wakiwa na mavazi yanayoonyesha mwili wao.

Joshua atakuwa na hamu kubwa ya kupata ushindi jijini Diriyah baada ya Ruiz kushangaza ulimwengu wa ngumi Juni kwa kumchapa Mwiingereza huyo katika raundi ya saba kwenye Ukumbi wa Madison Square Garden.

Mwanzoni ilikuwa inaonekana Joshua na Ruiz wangepigania Cardiff kabla ya Saudi Arabia kunyakuwa pambano hilo.

Joshua, tayari amewasili Saudia kwa lengo la kumalizia mazoezi yake ya mwisho kuelekea katika pambano hilo.  

Joshua alisema: 'Utakuwa ni usiku wa aina yake najua mashabiki wangu watakuwa hapa kwa ajili ya kuangalia pambano hili hasa wa kutoka Uingereza.