Breaking News
 

Owen atabiri sare Liverpool, Man City

Saturday January 13 2018

 

LONDON, ENGLAND. Nyota wa zamani wa Liverpool, Michael Owen ameweka utabiri wake kuhusu mechi za Ligi Kuu England zitakazopigwa wikiendi hii, huku akidai kwamba kipute cha Liverpool na Manchester City kitamalizika kwa sare huko Anfield.

Mechi hiyo kubwa itapigwa kesho Jumapili na Owen anadai kwamba timu hizo zitatoka sare ya 2-2, huku akidai kwamba matokeo ya mechi ya Chelsea na Leicester City, Antonio Conte na chama lake la The Blues atashinda 3-1 huko Stamford.

 Owen ametabiri pia mechi ya Crystal Palace na Burnley na kuwapa Palace ushindi wa 2-1, huku akidai Huddersfield na West Ham mechi yao itamalizika kwa sare ya 1-1 na Newcastle itaibika Swansea 2-1.

Watford watawapiga 2-0 Southampton, wakati West Brom watawachapa 1-0 Brighton, huku akiipa ushindi Tottenham mbele ya Everton kwa mabao 3-1.

 Arsenal watakaokuwa ugenini kwa Bournemouth, Owen amesema kwamba Arsene Wenger na timu yake itashinda 2-1, huku Manchester United watakaocheza Jumatatu, wametabiriwa kuishinda Stoke City huko Old Trafford licha ya kukiri kwamba Stoke wamekuwa na rekodi ya kutopoteza mechi yoyote ya ugenini waliocheza Jumatatu.