Ommy Dimpoz afichua nyuma ya pazia na Diamond

Thursday March 28 2019

 

By CHARITY JAMES

MKALI wa kibao cha You the Best, anayetambulika kwa jina la Ommy Dimpoz amesema hana tatizo na msanii mwenzake katika tasnia hiyo Naseeb Abdul 'Diamond' na kuweka wazi kuwa kilichowatenganisha ni kuwa katika usimamizi tofauti.
Hayo ameyasema leo katika ofisi za Mwananchi ambapo aliweka wazi kuwa hajawahi kufikilia kugombana na nyota huyo na siku ikitokea wakitaka kufanya kazi pamoja watafanya hivyo kiroho safi.
"Unajua ugomvi unatengenezwa na mashabiki mimi sijawahi kuwana ugomvi naye kilichopo sasa ni mimi kuwa katika usimamizi ya Rock Star na yeye kuwa katika kampuni yake hicho ndio kinachotutofautisha na sio kingine,"
"Ikitokea nikahitaji kufanya naye kazi nitafanya hivyo ila kwasasa acha maisha yaendelee na nawaomba mashabiki watambue kuwa sijawahi kugombana naye na sifikirii kuwa na ugomvi na msanii ambaye tunafanya kazi ya aina moja," alisema.
Akizungumzia kazi yake hiyo mpya alisema anamshukuru mungu inaendelea kufanya vizuri na imepokelewa vizuri tofauti na alivyokuwa anatarajia.

Advertisement