Ole amfanya Fergie apagawe Man United

Monday February 11 2019

MANCHESTER, ENGLAND .ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Sir Alex Ferguson kwenye kikosi cha Manchester United, Rene Meulensteen amefichua kuwa kocha huyo kwa sasa ana furaha kubwa kutokana na Ole Gunnar Solskjaer kuirudisha timu kwenye ubora wake.

Meulensteen hivi karibuni alitembelewa na Ferguson na kuzungumzia maendeleo ya Man United tangu Solskjaer alipochaguliwa kuwa kocha wa muda kwenye kikosi hicho.

“Amefurahi kutokana na kile Ole anachokifanya,” alisema Meulensteen akimzungumzia Fergie.

“Kwa sasa anaona kama vile ni yeye yuko kwenye usukani kwa kile kinachoendelea kwenye klabu. Sir Alex, ni kama mashabiki wengine wa timu hiyo, walikuwa kwenye hali mbaya kwa kipindi cha miaka mitano na nusu.

“Sir Alex anafurahishwa na Ole. Furaha kwa asilimia 100. Anafurahia mambo ya Ole. Anafurahi kwa jinsi United inavyocheza. Siku zote alikuwa akiwaambia wachezaji: ‘Nipeni kitu cha kushangilia. Kama mtaniburudisha, basi hapo mtakuwa mmewaburudisha mashabiki’. Ole amechukua hiyo na anaifanya Man United kwa sasa.”

Advertisement