Ole aelezea sakata la Greenwood

MANCHESTER, ENGLAND. ISHU kumbe ipo hivi, kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amefunguka juu ya kitendo chake cha kumuondoa kikosini staa wake, Mason Greenwood ambaye hakucheza kwenye mchezo na Newcastle ambapo Man United ilishida mabao 4-1 sambamba na ule wa PSG ambapo pia ilishinda mabao 2-1.

Ripoti zinadai mchezaji huyo amewekwa nje kama adhabu baada ya kuonekana akijirusha siku moja kabla ya mchezo wa Newcastle hali iliyosababisha kuchelewa kufika mazoezini lakini Ole amesisitiza mchezaji huyo hajajumuishwa kwa kuwa hana utimamu mzuri wa kimwili na sio sababu za nje ya uwanja.

“Siwezi kueleza kwa undani juu ya masuala ya kidaktari lakini ninnachojua ni Afya yake haikuwa sawa. Ingawa wikiendi ijayo anaweza kuwa sawa na atacheza,”alisema.

Greenwood na Foden ambao waliitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England waliondolewa kwenye kikosi hicho kilichocheza michuano ya Uefa Nations League dhidi ya Denmark sambamba na mchezo na Wales kwa sababu za kiutovu wa nidhamu, walivyoonesha wakiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa.

Baada ya kambi ya timu ya Taifa Solskjaer alitegemewa kuwa angemjumuisha kinda huyo kwenda St James’ Park kwa Newcastle, lakini badala yake alimpanga Daniel James.

“Mason hakuwa sawa ili kucheza, ndio maana tulimuacha na wala hakuna sababu nyingine za nje ya uwanja kama inavyosemwa na watu.