Nyumbani kwa MO bado hakijaeleweka

Thursday October 11 2018

 

Dar es Salaam. Hali ya taharuki imepanda nyumbani kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji, huku ndugu na familia wakishindwa kuzungumza lolote kuhusu suala hilo.

MCL Digital ilitembelea nyumbani kwa mfanyabiashara huyo nyumba kwake mtaa wa Libon na kuwakuta ndugu na jamaa na marafiki wakiwa hawana taarifa za usahihi juu ya ndugu yao.

Nje ya nyumba hiyo ulinzi ni mkali kupitia kampuni ya KK, lakini magari ya ndugu na jamaa wenye asili ya kihindi wamekuwa wakifika kujua kipi kinaendelea.

Baadhi ya ndugu hao wakigoma kutorekodiwa wamesema ndani kwa Mo hakuna taarifa sahihi kama amepatikana na kilichopo ni bado ndugu yao hajulikani aliko.

Wamesema wanasikia kuwa MO amepatikana, lakini wao wanaona katika mitandao, lakini walipouliza polisi wakakanusha kwamba hawana taarifa hiyo.

Baadhi ya ndugu zake waliofika hapo alianza kutokwa na machozi nyumbani hapo.

Advertisement