Nyota wa zamani Arsenal atua Villarreal

Wednesday August 8 2018

 

Madrid, Hispania. Kiungo wa zamani wa Arsenal, Santi Cazorla, amejiunga na Villarreal ya Hispania, kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao pia utakuwa na nyongeza yam waka mmoja.

Cazorla, aliitumikia Arsenal katika mechi 180 katika misimu sita aliyoitumikia kabla ya kuihama Mei mwaka huu baada ya mkataba wake kumalizika na kuondoka akiwa mchezaji huru.

Kiungo huyo mwenye miaka 33 anatarajiwa kutambulishwa rasmi kesho Alhamisi katika uwanja wa klabu hiyo wa Ceramica.

Kocha wa Villarreal, Javi Calleja, alisema anaamini mchezaji huyo atakuwa moja ya nguzo zao zitakazoiinua timu hiyo na kupata mafanikio kwenye Ligi Kuu Hispania.

 

Advertisement