Liuzio afunguka utajiri wake

Wednesday December 6 2017

 

By Dorice Maliyaga

Dar es Salaam. Staa wa Simba, Juma Liuzio kumbe pamoja na kuupiga mpira mwingi uwanjani, pia nje ya uwanja mambo yake siyo mchezo kabisa.
Mwandishi alifanya naye mazungumzo na kufunguka kuhusu ukweli wa mali zake kadhaa alizonazo baada ya kumkuta akiwa kwenye bajaji. Alipoulizwa kulikoni, akawa hana namna akafunguka ukweli wote kwamba ana bajaji.
Alisema pia, anazo pikipiki mbili za kukodisha maarufu kama bodaboda, zinamwingizia hesabu kila siku mbali na ile gari yake ya kutembelea aina ya Toyota  IST.