Nyota wa Chelsea Giroud aula Hollywood

Muktasari:

 

  • Mshambuliaji Olivier Giroud na beki Presnel Kimpembe waote kutoka Ufaransa wamelamba dume baada ya kuchaguliwa kuingiza sauti zao katika filamu maarufu duniani ya Spider Man, ambayo ipo katika hatua za mwisho kutoa toleo jipya.

London, England. Mshambuliaji anayehangaika kusaka mabao ndani ya Chelsea, Olivier Giroud, amelamba dili baada ya kuteuliwa kuigiza sauti ya Green Goblin katika filamu mpya ya Spider-Man. Giroud ambaye yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Ufaransa na beki wa Paris Saint-Germain wa Presnel Kimpembe ndio waliobahatika kulamba dili na kufanya kazi kwenye filamu hiyo inayotamba ndani ya Hollywood.

Waandaaji wa filamu hiyo wamesema kuwa wameamua kumtumia mshambuliaji huyo kwa kuwa kipande cha Green Goblin katika filamu hiyo inayo ya Spider-Man film kitazungumza katika lugha na lafidhi ya kifaransa.

Hata hivyo imeelezwa kuwa kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps hajafurahishwa na uamuzi wa kuwatumia wachezajin hao kwenye filamu hiyo ya Scorpion akiamini itawachanganya na kushindwa kuzingatia maelekezo yake kuelekea mechi ya Uefa Nations Ligi itakayocheza Ijumaa dhidi ya Uholanzi.

Kujitoa kwa washambuliaji Anthony Martial na Alexandre Lacazette walio majeruhi kunamfanya kocha wa Ufaransa kumtegemea mshambuliaji huyo pamoja na chipukizi Kylian Mbappe kupata ushindi dhidid ya Uholanzi.

Hata hivyo waratibu wa filamu hiyo walimtoa wasiwasi kocha huyo wakisema kwamba hawatawasumbua wachezaji hao hadi mechi hiyo imalizike.

Filamu hiyo inatarajiwa kuanza kuachiwa Desemba 12 mwaka huu lakini tayari baadhi ya vipengele vimanza kuachiwa ili kuitangaza ya filamu hiyo na sauti za Giroud na Kimpembe zikitarajiwa kuwavutia mashabiki katika nchi zinazozungumza Kifaransa.

Kwa mara ya kwanza filamu za Spider Man zilianza kuonekana mwaka 1957 na tangu wakati huo zimekuwa miongoni mwa filamu zinazopendwa na kuangaliwa na watu wengi zaidi duniani kote.