VIDEO: Ninje aula ukurungezi wa ufundi TFF

Muktasari:

Ninje amekuwa mkurungezi wa ufundi baada ya kuondoka nchini kutokana na kushindwa kuisaidia Kilimanjaro Stars kufanya vizuri katika mashindano ya Chalenji nchini Kenya.

Dar es Salaam.Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza kocha wa zamani wa Serengeti Boys, Ammy Ninje kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa Shirikisho hilo akichukua nafasi ya Salum Madadi.

Madadi aliondolewa katika nafasi hiyo mapema mwaka huu na kukaimiwa na Oscar Milambo ambaye baada ya uamuzi huu atarudi katika majukumu yake ya ukocha.

Ofisa habari wa TFF, Mario Ndimbo alisema kikao cha kamati tendaji ya TFF kilichokutana Jumamosi ya Oktoba 20 kilipitisha uamuzi wa kumteua Ninje.

"Ninje ndio atakuwa Mkurugenzi wa Ufundi kwa sasa na anatakiwa kuanza kazi mara moja kwani TFF inatambua anaishi Uingereza, lakini kuanzia sasa atarudi hapa nchini katika kituo chake cha kazi, " alisema.

"Leo Jumanne tutafanya tena na mkutano na kutoa taarifa za majukumu mapya ya makocha ambao watakwenda kuwa wa timu za Taifa ingawa Emmanuel Amunike ndio mkuu wa timu zote za Taifa," alisema Ndimbo.

Ndimbo alisema pia kamati tendaji imefanya mabadiliko ya baadhi ya kamati.

Kamati hizo kwa sasa zitakuwa hivi, Kamati ya Nidhamu, Kiomoni Kibamba, Peter Hella, Kassim Dau, Handley Matwenga na Twaha Mtengera.

Kamati ya madili, Richard Mbaruku, Thadeus Karua, Mussa Zangu, Benedict Nyagabona na Lugano Hosea.

Kamati ya Uchaguzi, Malangwe Ally, Mohammed Mchelengela, Benjamini Karume na Mohamed Gubati.

Kamati ya tiba, Paulo Marelle, Fred Limbanga, Norman Sabuni, Lisobina Kisongo, Billy Haonga na Violeth Lupondo.