Ni vita ya Man United vs Arsenal leo

Wednesday December 5 2018

 

England. Viwanja sita vya Ligi Kuu England vitawaka moto leo Jumatano usiku ambapo mechi ya Manchester United na Arsenal inaonekana kuwa na msisimko zaidi.

Timu zingine ambazo zitakuwa kibaruani leo, Burnley itawakaribisha Liverpool huku Everton itakuwa mwenyeji wa Newcastle United.

Mechi nyingine zitawakutanisha Fulham dhidi ya Leicester City. Pia Wolverhampton Wanderers watawakaribisha vigogo Chelsea huku Tottenham watakuwa Wembley wakiikaribisha Southampton.

Upande wa Kocha Unai Emery atakuwa na kazi ya kulinda heshima yake ya kutofungwa mechi 20 leo katika mashindano yote yaliyopita.

Emery amesema kwake hiyo ni mechi kubwa na kikosi chake kimejiandaa vyema huku akisisitiza wapo imara na watadhihirisha hilo uwanjani.

 

 

Advertisement