Ngorongoro Heroes wawaza ubingwa CECAFA

Muktasari:

  • Baada ya Ngongoro Heroes kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CECAFA, mahesabu yao kwa sasa ni kutwaa taji hilo kama alivyosema kocha mkuu wa timu hiyo, Zuber Katwila.

KOCHA wa Ngorongoro Heroes, Zuber Katwila amesema baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya CECAFA ya vijana chini ya umri wa miaka 20, sasa anawaza ubingwa.
Ngorongoro Heroes imefanya vizuri kundi B lililokuwa na timu ya Ethiopia, Zanzibar na Kenya imeshinda mechi zote katika michuano hiyo inayoendelea nchini Uganda.
Katwila alisema anaamini kikosi chake kwamba nina nafasi ya kutwaa ubingwa wa CECAFA na anajitahidi kuwajengea kujiamini, uzalendo wa kulibeba taifa lao.
"Wana ari ya kufanya maajabu katika michuano hiyo, kwanza nawatengeneza saikolojia zao kuwaaminisha kwamba wanavyofanya vyema ndivyo wanavyojitengenezea nafasi ajira zao dhidi ya wapinzani waocheza nao,"
"Soka ni ajira ambayo wao wamechagua ninachokifanya nikuhakikisha nawafanikisha ndoto zao, kikubwa nikuzingatia maelekezo yanayotakiwa, wakijua hilo basi hata ubingwa wa CECAFA ni rahisi kuuchukua ingawa kutakuwa na ushindani wa hali ya juu,"alisema.
Ngongoro inajiandaa kucheza mechi ya robo fainali dhidi ya wenyeji Uganda, mechi itakayochezwa kesho Jumapili saa 10 jioni, Gulu nchini Uganda