Hatima ya Ngoma mikononi mwa vigogo Yanga

Thursday December 7 2017

 

By KHATIMU NAHEKA

MABOSI wa Yanga wamekutana faragha na straika wao, Donald Ngoma katika vikao viwili tofauti ili kujadili utoro wake na Mzimbabwe huyo akajitetea kabla ya viongozi wake hao kumpa mtego ambao akishindwa kujinasua inakula kwake.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ni kwamba mabosi wa Yanga walikutana na Ngoma na kumtaka kuwasilisha taarifa zake za matibabu ya safari yake ya nchini kwao Zimbabwe kama kama hatawaridhisha basi safari ya kurudi kwao itamkuta.
Tayari Ngoma alishawasilisha taarifa hiyo, lakini Yanga wametaka kujiridhisha zaidi kwa kutaka uthibitisho kutoka kwa daktari maalum aliyegundua tatizo linalomsumbua kiasi cha kumfanya kushindwa kuitumia timu kwa muda mrefu.