Ngoma achomoa kiatu

Monday April 15 2019

 

By Charity James

KACHOMOA. Straika nyota wa Azam FC, Donald Ngoma amechomoa kiaina kwa kujitoa katika kinyang’anyiro cha Mfungaji Bora wa Ligi Kuu na kuamua kuwaachia kina Heritier Makambo wa Yanga, Salim Aiyee wa Mwadui na Meddie Kagere kwa madai ratiba inambana kwa sasa.

Aiyee ndiye kinara wa mabao kwa sasa akiwa na mabao 16 akifuatwa na Makambo mwenye 15 kisha Kagere aliyetupia mara 14, huku Ngoma akiwa na mabao yake 10 na ghafla jana Jumapili alitangaza kujiondoa kwenye mbio hizo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ngomaalisema tangu awali alikuwa hana mpango wa kuwania Kiatu cha Dhahabu msimu huu kutokana na majeraha aliyoanza nayo na kuweka wazi kuwa mpango wake ulikuwa ni kuvunja rekodi aliyomaliza nayo Yanga ya kupachika mabao 17.

“Kasi Yangu ya ufungaji ilikuwa inakwenda vizuri na nadhani ningefikia malengo, lakini napunguzwa kasi na kadi nilizopata ambazo zinanizuia kucheza baadhi ya mechi ikiwamo ya Mbeya City. Nilikuwa na kadi tatu za njano zilizotokana na mechi mfululizo, hivyo kupunguzwa kasi,” alisema Ngoma.

Advertisement