Neymar asherekea siku ya kuzaliwa na magongo

Muktasari:

 

  • Nyota huyo huenda akawa nje ya uwanja msimu huu wote kutokana  na kuumia kifundo cha mguu.

Nyota wa PSG, Neymar ambaye  mchezaji ghari duniani leo Jumanne tarehe 05 Februari anatimiza umri wa miaka 27, huku nyota huyo akiwa nje ya uwanja kutokana na kuuguza majeraha.

Neymar bado anauguza majeraha aliyoyapata  katika mechi yao ya Kombe la Ufaransa  wiki iliyopita. Neymar alisherehekea siku yake ya kuzaliwa jana Jumatatu asubuhi jijini Paris Ufaransa akiwa ametinga mavazi yenye rangi nyekundi pamoja na wapambe wake.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na wachezaji wanzake wa PSG na mastaa mbalimbali maarufu duniani.