Ndoa ya Wanyama, Migne yamalizika

Saturday September 29 2018

 

By Na VINCENT OPIYO

KOCHA wa Harambee Stars, Sebastian Migne ameshtuyshwa  na hatua ya nahodha Victor Wanyama kukosa kuwasili kwa mechi ya Ghana ya kufuzu kombe la mataifa bora barani mapema mwezi huu.

Katika mahojiano, Migne alikemea kiungo huyo kwa kukosa heshima akielezea alitaka aje ili afanyiwe vipimo huku ili kubaini jeraha lake ila Wanyama kasalia klabuni mwake Tottenham Hotspurs akiuguza jeraha la goti.

“Kama nahodha nilitaka aje awape vijana wenzake motisha kabla ya Ghana, pia ni sheria ambayo tumeweka kwamba kila mchezaji anayeumwa lazima aje timu ya taifa kwa vipimo zaidi pindi akiitwa,” alidai Migne wakati huo.

Hili liligonga vichwa vya habari na kuanza bifu mtandaoni baina ya mashabiki wengi wakidai Wanyama avuliwe unahodha kwa kukosa heshima na kocha wa timu ya taifa Migne ambaye aliizaba Ghana 1-0 na kurejea matokeo hayo dhidi ya Malawi kirafiki.

Sasa habari mpya ni kwamba ndoa hiyo shwari. Migne alifungasha virago kuelekea London mapema juma hili na kukutana na Wanyama kwa mazungumzo.

Kulingana na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), wawili hao walifanya mazungumzo ya faida kwa timu ya taifa na kocha Migne atazidi kutembelea wachezaji wanaosakata soka la kulipwa ughaibuni kabla ya mechi ijayo ya Ethiopia ambapo Stars wanahitaji ushindi kwa vyovyote kuimarisha nafasi za kujikatia tiketi ya mapema ya kuelekea Cameroon kwa fainali hizi. 

 

Advertisement