Ndemla, Mpilipi wana kazi Simba

Muktasari:

Katika  kipindi cha pili Mlipili aliingia kuchukua nafasi ya Joseph Peter wa kikosi B ambaye alionyesha ana kitu mguuni kwake kinachohitaji kupewa uzoefu.

KIUNGO wa Simba, Said Ndemla na beki Yusuph Mlipili wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ya kumshawishi kocha wao Patrick Ausssems ili kuwaamini kwenye kikosi chake cha kwanza.

Katika mechi inayoendelea Uwanja wa Taifa wawili hao  hawakuanza kikosi cha kwanza dhidi ya Bandari FC licha ya kwamba ni mechi ya kirafiki.

Kwa upande wa Mlipili bado ana kazi ya kufanya kwani kombinesheni ya Tairone Santos na Pascal Wawa imeonekana kuimarika kadri siku zinavyokwenda.

Kwa upande wa Ndemla ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na kuwepo viungo wengi wenye uwezo katika mchezo huo ambao ni Sharaf Shiboub na Francis Kahata.

Katika  kipindi cha pili Mlipili aliingia kuchukua nafasi ya Joseph Peter wa kikosi B ambaye alionyesha ana kitu mguuni kwake kinachohitaji kupewa uzoefu.

Endapo Peter ataendelea kupangwa na Aussems, basi anaonekana kucheza mpira aina ya beki anayeaminiwa kwenye kikosi cha kwanza Mohamed Hussein 'Tshabalala'.

Peter alikuwa anashindwa kukaba vyema kutokana na mastraika wa Bandari kuwa na miili mikubwa nakujikuta anaishia kunywang'anywa mpira pia alikuwa anapanda na kushuka.