Ndayiragije aanika watakaoivaa Burundi

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', Etienne Ndayiragije ametangaza kikosi cha wachezaji 25 watakaocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Burundi.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa, Oktoba 11 mwaka huu, mchezo huo ni kwa mujibu wa Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Akitangaza kikosi hicho leo Ijumaa, Oktoba 2, 2020 kwa niaba ya Ndayiragije, Mkuu wa Idara ya Habari ya TFF Clifford Ndimbo amesema, kikosi hicho kitaingia kambini Oktoba 5 tayari kwa mchezo huo.

Kikosi kikichotangazwa ni Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Yanga), Davis Kisu (Azam), Shomary Kapombe (Simba), Israel Mwenda (KMC), Mohamed Hussein (Simba) na Brayson David (Azam)

Wengine ni Bakari Mwamnyeto (Yanga), Abdallah Sebo (Azam), Dickson Job (Mtibwa), Iddy Mob (Polisi Tanzania), Jonas Mkude (Simba), Himid Mao (Enppi SC), Simon Msuva (Diffa), Ditram Nchimbi (Yanga), Feisal Salum na Ally Msengi (Stellenbosch).

Pia kuna Nahodha Mbwana Samatta (Fenefbache), John Bocco, Said Ndemla na Mzamiru Yassin (Simba), Idd Nado na Salim Abubakhar (Azam), Nickson Kibabage (Diffa) .