Namungo FC yatangulia TPL

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu alisema historia waliyoandika vijana wake imewapa heshima wakazi wa Rungwa na sasa wajiandae kushangilia na kuona nyota kadhaa wa Ligi Kuu msimu ujuao.


NAMUNGO FC imekuwa timu ya kwanza kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya jioni ya jana Jumatatu kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Mawenzi Market mjini Morogoro.

Namungo imepanda TPL kutoka Kundi A baada ya kukusanya alama 40 ambazo zitafanya zisiweze kufikiwa na klabu nyingine za kundi hilo, huku ikisubiri alama tatu za dezo baada ya Friends Rangers kususia pambano lao lililopita huku wakiwa washapigwa mabao 2-0. Mabao ya Namungo yamefungwa na Abeid Athumani na Reliant Lusajo huku lile la Mawenzi likifungwa na Ofein Francis.

Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu alisema historia waliyoandika vijana wake imewapa heshima wakazi wa Rungwa na sasa wajiandae kushangilia na kuona nyota kadhaa wa Ligi Kuu msimu ujuao.

“Michezo ya FDL imeleta changamoto kubwa kwa wachezaji wetu lakini tumepambana vilivyo.”