Namungo FC yaandika rekodi

Muktasari:

Namungo katika kuweka mabo sawa ilisafisha benchi lake la ufundi kwa kumtoa Fulgence Nolvatus na kumkabidhi timu Hitimana Thiery pamoja na Bakari Malima 'Jembe Ulaya'.
 

BAADA ya kufanikiwa kupanda kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, uongozi wa Namungo FC umesema umeandika historia kubwa kwao pamoja na kukutana na ushindani mkubwa katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Namungo imekuwa timu ya kwanza kupanda daraja ikiwa imeandika historia ya kufungwa mchezo mmoja pekee ilipolala mbele ya Dar City kwa kufungwa mabao 2-1 na na sasa ligi hiyo imesalia michezo miwili huku Namungo ikiweka kibindoni alama 40 huku ikisuburi hatima ya mchezo waoi dhidi ya Friends Rangers uliovunjika wakiwa wanaongoza 2-0 kwenye Uwanja wa Majaliwa Mjini Ruangwa.
Akizungumnza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Namungo, Hassan Zidadu alisema historia waliyoandika vijana wake imewapa heshima wakazi wa Rungwa na sasa wajiandae kushangilia na kuona nyota kadhaa wa Ligi Kuu msimu ujuao.
"Michezo ya FDL imeleta changamotoi kubwa kwa wachezaji wetu kutokana na ugumu wa ligi ulivyokuwa na tunaamini ushindani huo utaendelea hata kwenye TPL msimu ujao tutakaposhiriki," alisema Zidadu.
Mabao ya Namungo yaliwekwa kambani na Abeid Lusajo wakati lile la kufutia machozi la Mawenzi likifungwa na Offein Francis.
Namungo katika kuweka mabo sawa ilisafisha benchi lake la ufundi kwa kumtoa Fulgence Nolvatus na kumkabidhi timu Hitimana Thiery pamoja na Bakari Malima 'Jembe Ulaya'.