Naldo aitamani rekodi City

Muktasari:

Ambokile ndiye aliyekuwa akiongoza kwa mabao akifunga mabao 10 kabla ya kutimkia Afrika Kusini kujiunga kwa mkopo na Black Leopards, lakini bao la Naldo dhidi ya Coastal lilimfanya amnase straika huyo.

STRAIKA wa Mbeya City, Idd Seleman ‘Naldo’ juzi kati alifunga bao lake la 10 katika Ligi Kuu Bara na kumnasa, Eliud Ambokile aliye nje ya timu hiyo kwa sasa, lakini amesisitiza anataka kuvuka idadi ya mabao hayo ili aweke rekodi klabuni hapo.

Ambokile ndiye aliyekuwa akiongoza kwa mabao akifunga mabao 10 kabla ya kutimkia Afrika Kusini kujiunga kwa mkopo na Black Leopards, lakini bao la Naldo dhidi ya Coastal lilimfanya amnase straika huyo.

“Malengo yangu mwanzoni nilitaka kuwania kiatu cha dhahabu, ila nimeshindwa kufikia malengo, nataka kutumia mechi tatu zilizosalia kuvunja rekodi na kuisaidia timu yangu kupata matokeo,” alisema Naldo.