Nado: Washambuliaji tunadeni kubwa Azam

Wednesday August 14 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam.Mshambuliaji wa Azam FC, Idd Seleman 'Nado' amesema safu yao ya ushambuliaji inakazi kubwa ya kufanya kuhakikisha wanashinda mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kanema.

Azam walipoteza mchezo wao wa kwanza Kombe la Shirikisho ugenini kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 na wanatarajia kurudiana na wapinzani wao kati ya Agosti 20 hadi 23 mwaka huu.

Nado alisema sababu kubwa iliyowaangusha ugenini ni safu yao ya ushambuliaji kukosa umakini katika mipira ya umaliziaji huku akibainisha kuwa walitengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha pili, lakini walishindwa kuzitumia.

Alisema hilo kocha wao aliliona na ndio analolifanyia kazi zaidi kwa muda huu uliobaki na kuongeza kuwa kuelekea mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba watahakikisha wanapambana kusawazisha makosa yao kwa kufunga mabao mengi.

"Tunakutana na Simba kabla ya mchezo wa marudiano na Fasil Kanema ni kipimo sahihi kwetu kwani Simba ni klabu nzuri na wao pia wapo katika mashindano makubwa ya kimataifa na wanamchezo nyumbani kama sisi japo wao wanafaida ya kutoruhusu nyavu zao kutikishwa," alisema Nado.

Advertisement