Mzee Akilimali apiga ‘push up’ kuthibitisha yupo fiti

Friday March 15 2019

 

By CHARITY JAMES

KATIBU wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga, mzee Ibrahim Akilimali amewajibu kwa kupiga ‘push up’ wanaomzushia ugonjwa na  kusambaza taarifa kwa Watanzania kuwa anahitaji misaada.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mzee Akilimali amesema hana tatizo lolote yupo fiti kiafya na wanaomzushia ugonjwa huo anampango wa kuwashtaki na kuweka wazi kuwa hahitaji msaada wowote kwani anajiweza kwa kila kitu.

Alisema ili kuwaaminisha Watanzania na kuwapuuza hao wanaosema yeye ni mgonjwa ameamua kutoka Bagamoyo ambako ndio alikuwa na amekuja Dar es Salaam ili kuwathibitishia Watanzania wote wanaothamini umuhimu wake katika klabu ya Yanga.

"Sina tatizo lolote kiafya naomba niwathibitishie Watanzania kwa kupiga pushapu na naomba muwafikishie taarifa hao wanaonichafua kutwa kuwa mimi ni mgonjwa. Nahitaji misaada na nipo katika michakato ya kuwashtaki hao wanaonitangazia ugonjwa."

"Nawapa wiki tatu kuniomba radhi wamewaongopea watu kwamba mimi naoumwa taabani na ninaomba misaada. Sasa nawaomba watumie vyombo vyao hivyo hivyo walivyonitangazia kukanusha taarifa hizo na kuniomba msamaha," alisema Mzee Akilimali.

 

 

Advertisement