Mwinyi Zahera anamaliza na Bocco, Kagere

Muktasari:

Bocco amefunga mabao 14, kwenye Ligi Kuu Bara sawa na yale ambayo amefunga msimu uliopita, lakini Kagere ndio kinara wa mabao kwenye msimamo wa wafungaji akifikisha mabao 20.

KOCHA wa Yanga Mkongomani Mwinyi Zahera, ameshindwa kujiuia na kueleza kuwa msimu huu mbali ya kikosi chake kufanya vizuri kuna baadhi ya wachezaji kutoka timu nyingine wamefanya vizuri zaidi msimu huu.
Zahera alisema, katika orodha yake ya wachezaji waliofanya vizuri msimu huu wapo wawili na wanatoka Simba ambao ni Mnyarwanda Meddie Kagere na nahodha John Bocco.
"Katika timu yangu wote wamefanya vizuri ndio maana tuliweza
kuongoza Ligi Kuu kwa muda mrefu na tukafanya vizuri katika
mashindano mengine," alisema Zahera.
"Hawa washambuliaji wawili, Kagere na Bocco wamefanya vizuri
msimu huu kwangu kama kocha nimewaona. Si kama wengine
hawakufanya vizuri hapana, walifanya hivyo lakini hawa wawili ni
hatari," alisema Zahera kwa ufupi.
Mpaka sasa Bocco amefunga mabao 14, kwenye Ligi Kuu Bara sawa na yale ambayo amefunga msimu uliopita, lakini Kagere ndio kinara wa mabao kwenye msimamo wa wafungaji akifikisha mabao 20.