Mwigulu aibua shangwe Kubwa Kuliko

Muktasari:

Nchimbi ambaye ni mwanachama na mdau mkubwa wa Yanga akiwa ndani ya Singida United pia alifanikisha usajili wa kiungo Feisal Salum akitokea JKU.

MWANACHAMA wa klabu ya Yanga, Mwigulu Nchemba ameibua shangwe kwa wanachama wenzake waliojitokeza ukumbi wa Diamond Jubilee kwenye hafla ya Kubwa Kuliko iliyoandaliwa na klabu hiyo kwa lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Nchemba ambaye pia ni Mkurugenzi wa klabu ya Singida United, alifika ukumbini akiwa amevalia jezi ya Yanga na ndipo shangwe hizo zilianza baada ya kumuona.
Nchimbi ambaye ni mwanachama na mdau mkubwa wa Yanga akiwa ndani ya Singida United pia alifanikisha usajili wa kiungo Feisal Salum akitokea JKU.
MAKAME NDANI
Wakati sherehe za ufunguzi zikiwa zinaendelea mnamo saa 6:40 mchana kiungo mpya wa Yanga, Abdulaziz Makame aliingia ukumbini kuungana na wanachama kwenye hafla hiyo.