Mwendwa, Karia wapewa Afcon, Cecafa yaiteka CAF

Muktasari:

Karia ni mwenyekiti wa CECAFA na Mwendwa, wataungana na Bosi wa soka nchini Burundi, Reverien Ndikuriyo kwenye kamati hiyo itaongozwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Nairobi. Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF), limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Nick Mwendwa na mwenzake wa Tanzania, Wallace Karia katika kamati ya kuandaa mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON2021).

Karia mwenyekiti wa CECAFA na Mwendwa, wataungana na Bosi wa soka nchini Burundi, Reverien Ndikuriyo kwenye kamati hiyo itakayongozwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Ahmad, atasaidiwa na bosi wa soka nchini Senegal, Augustin Senghor. Aidha, Boss wa shirikisho la soka nchini Uganda (FUFA), Moses Magogo yeye amesalia katika wadhifa wake wa uenyekiti wa mchezo wa Futsal na Beach Soccer, akisaidiwa na Ali Harred Mohamed wa Djibouti.

CAF pia imeteua kamati ya mashindano ya CHAN, ambapo wajumbe wake wengi wanatokea kwenye nchini wanachama wa CECAFA. Wajumbe hao ni Aruna Moses Mawanda (Uganda), Younisse Yassin Mohamed (Djibouti), Isayas Jira Bosho (Ethiopia)

Abraham Esayas (Eritrea), Hassan Bargo (Sudan), Francis Amin Michael (South Sudan), Hassan Mohamed Mahmoud (Somalia) na Jean Damascene Sekamana wa Rwanda. Huku Jean Sseninde wa Uganda, Lydia Nsekera (Burundi) na Kessy Lina (Tanzania), wakiteuliwa katika kamati ya Soka la wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, zilizoifikia Mwanaspoti, ni kwamba, wajumbe wengine wa ukanda huu wa CECAFA, pia wameteuliwa kujaza nafasi mbalimbali kwenye kamati za CAF.

Wajumbe hao ni Abnet Meskel (Ethiopia), Mohamed Galal (Sudan), Abdel Moneim Moustafa Hussein (Sudan), Jeremie Manirakiza (Burundi), haile Woldemicael (Eritrea), Anthony Otto (South Sudan), Paul Gasper Marealle (Tanzania), Mustapha Samugabo (Burundi), Ali Mohamed Ahmed (Somalia) na Garang Maper Dut (South Sudan).