Mwasekaga awaza haya Singida United

Muktasari:

Licha ya Singida United kuburuzwa mkiani, haijawavunja moyo wachezaji kuendelea kupambana kuona wanaambulia ushindi kwa mechi zilizosalia.

MSHAMBULIAJI wa Singida United, Six Mwasekaga amesema licha ya upepo mbaya uliowakumba wa kuambulia vichapo katika mechi mfululizo, wanajipa matumaini ya kumaliza kwa ushindi michezo iliosalia.

Mwasekaga amekiri kuumizwa na matokeo mabaya ambapo wamecheza mechi 23, kushinda mbili, sare tano na kufungwa kufungwa 16, huku wakivuna pointi 11 kwamba ni kitu kibaya.

"Ingawa sisi tumeingia dirisha dogo, hatuwezi kufurahishwa na hali mbaya ya timu ndio maana nasema tutapamba kwa kadri tutakavyoweza ili kuhakikisha tunashinda mechi zilizopo mbele yetu,"

Ameongeza kuwa "Hatuwezi kukata tamaa mpaka dakika ya mwisho, ingawa tunatambua kwamba tuna wakati mgumu kuliko wenzetu ambao wapo juu kwenye msimamo wa ligi," amesema.