Wema Sepetu ataja mambo aliyoyachukia mwaka 2019

Friday January 3 2020

Mwanaspoti-Wema Sepetu-ataja mambo-Tanzania-Miss-aliyoyachukia-mwaka 2019

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam. Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu Kupitia Application yake ya #WemaApp ameyataja mambo yaliyochukia zaidi kwa mwaka 2019

Wema ameorodhesha mambo ni kesi yake ya kushitakiwa kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani.

Pia aliorodhesha kukaa muda mrefu bila kufanya kazi, kifo cha kaka yake na kuwekwa rumande kwa wiki moja kwa kosa la kutoudhuria mahakamani.

Hata hivyo Wema toka amalize kesi yake ya kushitakiwa kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani, amekuwa mtu wa kujiepusha vitu vingi husasan kuonekana katika sehemu za starehe pamoja na kuposti vitu vinavyohusu kazi zake katika akaunti yake ya instagram.

Wiki chache zilizopita Wema aliimbia Mwanaspoti kuwa malengo yake ya mwaka 2020, ni kuwa mtu wa tofauti kwa kutekeleza mipango yake aliyojiweka juu ya maisha.

 

Advertisement

 

Advertisement