Kipa Dida amefungua milango ya kutua Lipuli

Wednesday January 8 2020

Mwanaspoti-Tanzania-Kipa Dida-Simba SC-amfungua-Lipuli-milango-Ligi Kuu-kutua Lipuli

 

By CHARITY JAMES

Dar es Salaam. Uongozi wa Lipuli FC ipo katika hatua nzuri za kuinasa saini ya aliyekuwa kipa wa Simba, Deogratus Munish 'Dida' katika dirisha hili la usajili.

Dida amemaliza mkataba wake na Simba, tangu msimu huu hakuwana timu ya kucheza muda mwingi alikuwa akifanya shughuli za kilimo nyumbani kwao mkoani Kilimanjaro pamoja na kufanya mazoezi na timu ya beach soccer.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dida alikiri kuwepo kwa mazungumzo hayo baina yake na uongozi wa Lipuli kwa kubainisha kuwa mambo yatakapokuwa sawa ataweka wazi kilakitu.

"Nikweli nimefanya mazungumzo na uongozi wa Lipuli kwa njia ya simu natarajia kukutana nao kwaajili ya makubaliano mambo yakienda sawa nitakuwa na cha kuzungumza kwasasa naomba kupewa muda," alisema.

"Siwezi nikakwambia tumemalizana wakati makubaliano kuhusiana na fedha ya usajili hatujafanya yawezekana tukashindwana nao na nikakupotosha naomba usubiri hiyo kesho ‘leo’ ndio utapata uhakika kama nitakuwa mali ya timu hiyo," alisema Dida.

Advertisement