TID ‘Mnyama’ akerwa kuitwa msanii mkongwe

Wednesday November 13 2019

Mwanaspoti-TID-Mnyama-Tanzania-muziki-akerwa-kuitwa-msanii-mkongwe

 

By Nasra Abdallah

Dar es Salaam.Mwanamuziki TID amesema anakerwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaita wasanii wa enzi zao kuwa ni wakongwe.

TID ameyasema hayo leo Novemba 12, 2019 katika mahojiano maalum walipotembelea ofisi za Mwananchi akiwa ameambatana na wasanii wenzake Mandojo na Domokaya.

Akizungumza kwenye kipindi cha MCL Extra msanii huyo aliyewahi wimbo wa ‘Zeze’ na ‘Nyota yangu’, amesema kuwaita wao kuwa ni wasanii wakongwe ni kutaka kuwatenga na muziki wa kizazi kipya jambo ambalo anaona si sawa.

“Mnatuitaje wakongwe wakati muziki huo hauna hata miaka 40 hivyo unaposema muziki wa kizazi kipya na sisi tupo ndani yake

 “Maana ya muziki wa kizazi kipya ni muziki wa sasa, sasa iweje wasanii wake waitwe wakongwe hizo ni chuki na sumu ambazo watu wanataka kuzieneza ili kututenga na muziki huo.

“Kwani sisi wote ni wasanii tunaotakiwa kupewa haki sawa kuanzia kwenye malipo na upatikanaji wa kazi zake,” amesema msanii huyo huku akiungwa mkono kauli yake hiyo na Mandojo na Domo Kaya.

Advertisement

Pia wasanii hao wamesema katika kuunganisha nguvu kusukuma muziki wao wameamua kuunda umoja wao,  ambao watakuwa wakifanya kazi kama timu huku moja ya kazi wanayoiandaa ni kuandaa tamasha lao kwa kuzunguka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Advertisement