Sven aishtukia Azam, awaita fasta wakina Kagere Zanzibar

Muktasari:

Simba imefuzu kwa nusu fainali baada ya kuichapa Zimamoto 3-1, sasa itacheza dhidi ya Azam iwapo itafanikiwa kushinda basi uenda ikakutana na Yanga au Mtibwa Sugar katika fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Dar es Salaam. Baada ya Simba kufuzu kwa nusu fainali Kombe la Mapinduzi utakiwa kucheza na Azam FC kesho Alhamisi kocha wa Sven Vandenbroeck amevunje mapumziko ya nyota wake aliowaacha Dar es Salaam kwa kuwaita haraka Zanzibar.

Simba imefuzu kwa nusu fainali baada ya kuichapa Zimamoto 3-1, sasa itacheza dhidi ya Azam iwapo itafanikiwa kushinda basi uenda ikakutana na Yanga au Mtibwa Sugar katika fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Simba iliamua kuwaacha nyota wake wote waliocheza katika mchezo dhidi ya Yanga, huku ikiwatumia wachezaji wa akiba na wale wa vijana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi.

Mwanaspoti linafahamu nyota waliokuwa wamebaki Dar es Salaam leo asubuhi wameanza safari kwaajili ya mchezo wa nusu fainali wakiondoka na usafiri wa boti.

Simba inajua ugumu wa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ambao ndiyo mabingwa watetezi.

Mchezo huo unakuwa wa kulipa kisasi katika fainali za Mapinduzi baada ya mwaka jana Azam kuifunga Simba 2-1 na kuchukua kombe hilo.

Simba na Azam Fc zitacheza nusu fainali ya pili Ijumaa huku nusu fainali ya kwanza ikichezwa Alhamis kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar na michezo yote ikichezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja.