Sven: Simba inataka pointi tatu tu kwa Mbao

Muktasari:

Simba vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanashuka uwanjani kusaka pointi tatu wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na Mtibwa Sugar.

Mwanza.Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema licha ya kuwakosa baadhi ya nyota wake anaamini atapata ushindi katika mchezo wao wa kesho Alhamisi dhidi ya Mbao kwenye Uwanja CCM Kirumba.

Simba vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanashuka uwanjani kusaka pointi tatu wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na Mtibwa Sugar.

Wachezaji wanaoweza kukosa mchezo huo ni kiungo Mzamiru Yassin, Deo Kanda na Miraji Athuman walioumia katika mechi zilizopita.

Akizungumza kabla ya mazoezi yao, Sven amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanashinda mechi hiyo.

“Naamini mchezo utakuwa na ushindani, lakini kutokana na lengo lake ni kuhakikisha wanashinda na kuondoka na pointi tatu.

Alisema mazoezi waliofanya leo yatasaidia sana katika kufikia malengo yao na kwamba matokeo ya Zanzibar wameshayasahau na sasa akili ziko kwenye mchezo wa kesho.