Samatta apewa jezi namba 20 Aston Villa

Tuesday January 21 2020

Mwanaspoti-Samatta-apewa-jezi-namba 20-Aston Villa-Mwanasport-Michezo-MICHEZO

 

London, England. Mshambuliaji Mbwana Samatta sasa atakuwa akivaa jezi namba 20 katika klabu yake mpya ya Aston Villa.

Samatta aliyejiunga na Aston Villa na kuchagua jezi namba 20 ikiwa ni tofauti na ile aliyokuwa akivaa Genk iliyokuwa namba 10.

Samatta alikuwa na huru wa kuchagua namba zilizokuwa hazina watu kuanzia namba 2, 16, 19, 20, 29, 31-32, 33, 35-37 na 38.

Katika namba hizo Samatta amechagua namba 20, wakati alipojiunga kwa mara ya kwanza Genk nahodha hiyo alipewa jezi 77 mwenyewe akisema hataki matatizo na wenye namba wengine.

Hata hivyo kiwango bora alichokionyesha katika klabu hiyo ya Ubelgiji ilifanya Samatta kupewa jezi namba 10 aliyodumua nayo hadi anaondoka.

Samatta amejiunga Aston Villa kuziba pengo la Mbrazili Wesley Moraes aliyeumia na atakuwa nje kwa msimu mzima.

Advertisement

Advertisement