Sabato aikacha Gwambina atua zake Kagera Sugar

Tuesday January 7 2020

Mwanaspoti-Sabato-aikacha-Tanzania-Gwambina-Kagera Sugar-Ligi Kuu-Soka- usajili

 

By THOMAS NG’ITU

Dar es Salaam.Mshambuliaji Kelvin Sabato ‘Kiduku’ ameachana na klabu yake ya Gwambina FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, na kujiunga na Kagera Sugar.

Sabato amejiunga na Kagera Sugar kwa mkataba wa miezi sita baada ya viongozi wa pande mbili kukaa chini na kufikia mwafaka.

Kusajiliwa kwa Sabato katika kikosi cha Kagera Sugar kutafanya eneo la ushambuliaji katika kikosi hiko kuongezeka vita kwani hivi sasa yupo Yusuph Mhilu mwenye mabao 5, Frank Ikobela na Evaristy Mujwahuki ambaye ni majeruhi.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa Mtibwa Sugar, anasifika kwa uwezo wa kutumia nguvu kupambana na mabeki pia uwezo wake wa kupiga mashuti yanayolenga goli.

Sabato alisajiliwa mwanzoni mwa msimu baada ya Uongozi wa Gwambina kuamua kusajli nyota wengi kutoka Ligi Kuu kama Raizin Hafidh, Jacob Masawe na Malika Ndeule.

Advertisement