Ommy Dimpoz: Nandy alinivuruga katika wimbo wa Kata

Thursday January 9 2020

Mwanaspoti-Ommy Dimpoz-Nandy-Tanzania-alinivuruga-katika-wimbo wa Kata

 

By RHOBI CHACHA

Dar es Salaam.Mwanamuziki Ommy Dimpoz amesema haikuwa rahisi kufanya video wimbo wake mpya 'Kata' aliomshirikisha Nandy.

Ommy amesema Nandy ni msichana anayemvutia mwanamume yeyote unapokuwa naye karibu.

“Ilikuwa mtihani kidogo unajua kufanya kazi na msichana mrembo ushawishi unakuwa mwingi. Kwahiyo nilikuwa najizuiazuia,” amesema Ommy

“Kwa sababu kwenye video kuna mambo mengi, mtu anaweza akatokea akabidilisha nguo mbele yako, kwahiyo yote niliyavumilia, ni lazima uvumilie majaribu ili kazi iende,” amesema Dimpoz.

Aidha muimbaji huyo amesema kutokana na picha za video wa wimbo huo zilianza kusambaa mwaka mpya kwenye akaunti ya Ommy Dimpoz ya Instagram na kuzua minong'ong'ono kwa baadhi ya watu hadi kujitetea sio za mapenzi bali wako kazini mjini Mombasa Kenya kwenye scene ya video yake mpya.

Video wa wimbo wa Kata iliyoachiwa siku tano zilizopita imeshika namba tatu katika mtandao wa YouTube ambapo siku mbili zilizopita ilikuwa namba moja.

Advertisement

Ommy Dimpoz mara ya mwisho kuonekana kafanya ngoma na Msanii wa kike Tanzania ilikua zaidi ya miaka mitano iliyopita alipoidondosha ‘me and you’ na Vanessa Mdee.

Advertisement