Habari njema Kenya! Mo Salah aikosa Harambee Stars leo

Thursday November 14 2019

Mwanaspoti-Mo Salah-Kenya-aikosa-Harambee-Stars-Misri-Afcon-Cameroon

 

By Thomas Matiko

WINGA matata wa Misri, Mo Salah hatashiriki kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Harambee Stars leo kwenye mechi ya kufuzu kwa dimba la AFCON 2021 baada ya kuteguka mguu.
Zitakuwa habari njema kwa kocha wa Stars Francis Kimanzi hasa kutokana na makali ya Salah.
Fowadi huyo alipata jeraha hilo kwenye mechi ya Ligi Kuu England wikendi iliyopita dhidi ya Manchester City na alitupia bao moja kwenye ushindi wao wa mbao 3-1.
Mechi hiyo itachezewa mjini Alexandaria Misri. Licha ya jeraha hilo, Salah na nahodha wa Stars Victor Wanyama anayekipiga pale Tottenham Hotspurs walisafiri kwenye ndege moja kutoka England hadi Cairo.
Japo Kimanzi atakuwa na unafuu wa kukosekana kwa Salah, mwenyewe ana homa kwani hatazipata huduma zake straika John Aviire ambaye wameachwa kutokana na sababu za kibinfasi.
Kocha Kimanzi ameamua kuwabeba mastraika Miachel Olunga anayesumbua kule Japan, Jesse Were anatekipiga Zambia na kinara wa mabao kwa sasa kwenye ligi ya KPL John Makwatta wa AFC Leopards.
Baada ya kuchafuana na Misri, Stars watakipiga dhidi ya Togo Jumatatu katika uwanja wa Kasarani Nairobi.

Advertisement