Malinzi atiwa hatiani kwa kutengeneza nyaraka za uongo

Muktasari:

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Desemba 11, 2019 imemtia hatiani aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Desemba 11, 2019 imemtia hatiani aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo.

Mbali na Malinzi, mwingine aliyetiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo ni aliyekuwa katibu wa shirikisho hilo, Cestine Mwesigwa

Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya

Katika shtaka hilo Malinzi anadaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edgar Masoud aliwekwa Mwanga.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.

Kesi hiyo bado inaendelea