Kisa Kagere, Okwi: Simba yaifunika Yanga tuzo Afrika

Muktasari:

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Tanzania kutoa wachezaji wawili tangu CAF ilipoanzisha utaratibu wa kutoa tuzo kwa wachezaji wanaocheza klabu za barani humu.

Dar es Salaam. Simba imeipiga bao la mwaka Yanga baada ya kuwa klabu ya kwanza ya Tanzania wachezaji wawili Meddie Kagere na Emmanuel Okwi kuingia katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo Mwanasoka wa bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza Afrika.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika, Simba imekuwa moja timu tano zilizoingiza wachezaji zaidi ya mmoja wakiongozwa na mabingwa Esperance ya Tunisia iliyoingia nyota wa tano.

Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ameingia katika kinyang’anyiro hicho baada ya kufunga mabao sita na kuisaidia timu hiyo kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali ya Kagere nyota mwingine wa Simba aliyeingia katika orodha hiyo ni Okwi aliingoza Simba kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kabla ya Mganda huyo kuondoka na kujiunga na Al Ittihad ya nchini Misri mwisho wa msimu huu.

Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Tanzania kutoa wachezaji wawili tangu CAF ilipoanzisha utaratibu wa kutoa tuzo kwa wachezaji wanaocheza klabu za barani humu.

Mtanzania Mbwana Samatta alitwaa tuzo hiyo mwaka 2015, akiwa na klabu ya TP Mazembe, pia kipa wa Uganda, Denis Onyango mshindi wa mwaka jana ameingia katika orodho hiyo kutetea taji lake.

Mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza Afrika

· Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)

· Anice Badri (Tunisia & Esperance)

· Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

· Emmanuel Okwi (Uganda & Simba)

· Ferjani Sassi (Tunisia & Zamalek)

· Fousseny Coulibaly (Cote d'Ivoire & Esperance)

· Franck Kom (Cameroon & Esperance)

· Herenilson (Angola & Petro de Luanda)

· Ismail El Haddad (Morocco & Wydad Casablanca)

· Jean Marc Makusu (DR Congo & AS VITA)

· Kodjo Fo Doh Laba (Togo & RS Berkane / Al Ain)

· Mahmoud Alaa (Egypt & Zamalek)

· Meddie Kagere (Rwanda & Simba)

· Meschack Elia (DR Congo & TP Mazembe)

· Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance)

· Tarek Hamed (Egypt & Zamalek)

· Themba Zwane (South Africa & Mamelodi Sundowns)

· Trésor Mputu (DR Congo & TP Mazembe)

· Walid El Karti (Morocco & Wydad Casablanca)

· Youcef Belaïli (Algeria & Esperance / Ahli Jeddah)