Reinhardt kocha wa Harambee Stars aliyebamba kwa kupenda mavipindi

Muktasari:

Huyu ni kocha aliyebamba kinoma alipoifunza Harambee Stars kuanzia miaka ya 1980 kiasi cha mashabiki kuanza kumsukuma achukue uraia wa Kenya na kisha ikibidi agombee urais wa nchi hii.

Nairobi, Kenya. IKIWA kuna kocha mmoja atakayesalia kuwa kumbukumbu kwa wadau wengi wa soka hapa nchini, basi atakuwa ni Mjerumani Reinhardt Fabish.
 Fabishi amekwishafariki dunia.
Huyu ni kocha aliyebamba kinoma alipoifunza Harambee Stars kuanzia miaka ya 1980 kiasi cha mashabiki kuanza kumsukuma achukue uraia wa Kenya na kisha ikibidi agombee urais wa nchi hii.
Tukiwa tunatimiza mwongo leo ikiwa ni siku ya mwisho kabisa ya 2019, hakuna kocha ambaye katokea katika kipindi hicho hapa nchini na kuweza kubamba kwa kufanya alichofanya Fabish.
Ni kocha aliyewabamba wengi sana na kuifanya soka na timu ya taifa Harambee Stars kwa ujumla kuwa maarufu nchini.

KIFO
 Julai 12, 2008 ndio siku ya mwisho aliyovuta pumzi zake za mwisho Fabisch kabla ya kutangulia mbele za haki.
Fabish aliyeifunza Stars 1987, 1997 na 2001-2002, alifariki dunia miaka 11 iliyopita akiwa nyumbani kwao Ujerumani baada ya kulemewa na ugonjwa wa saratani uliokuwa umemhangaisha kwa miaka mingi mno.
Kocha huyo aliyewahi kuichezea Borussi Dortmund (1969-71) aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 57.

ALIVYOBAMBA
Fabisch ndiye  kocha wa pekee atakayekumbukwa kuwa mwenye mafanikio makubwa ya kisoka nchini alipoifuinza Harambee Stars.
Mchango wake katika soka la Kenya ulikuwa mkubwa. Fabish alifutwa kazi akirudishwa mara tatu pale Stars. Mzungu huyu alijitosa kwenye soka la Kenya katika kipindi ambacho kila kitu kilitawalia na siasa. Rais Dikteta Daniel Moi ndiye aliyekuwa madarakani enzi hizo na chochote kile kilichokuwa kikifanyika nchini, kilistahili kumsifia au kwenda namna alivyotaka yeye.
Hata wasanii hawakuwa na uhuru wa kutunga nyimbo za kusifia upinzani au kumpomnda rais kama ilivyo sasa. Siasa hizi pia ziliathiri soka wakati huo. Fabish akaamua kuwa mwelewa.

ALIPENDA MADRAMA
Drama zake za nje na ndani ya uwanja zinaweza kufananishwa na vimbwanga vya kocha Jose Mourinho.
Fabish alipenda sana kuzua mavipindi zilizoishia kunogesha mchezo na kuifanya Stars kuwa maarufu sana miongoni mwa umma.
Vimbwanga vya Fabish vilimgeuza kipenzi cha wengi sana  kiasi cha kuzua vuguvugu ndogo la mashabiki  lilioanza kumsukuma kuchukua uraia wa Kenya ili  agombee urais lengo likiwa ni  kumwondoa madarakani Rais mstaafu Moi aliyekuwa amewachosha wengi na uongozi wake wa kiimla. Hii inakuonyesha ni jinsi gani Fabish alivyovuta ushawishi hapa nchini. Hakuna kocha mwingine aliyefanikiwa kupata umaarufu kama huu.
Wakati akitua Kenya, hakuna shabiki yeyote  mwenye ujasiri wa aina gani angeliweza kunyanyua bango lenye maandishi ‘Fabisch For President’ kutokana na uongozi wa kidkteta wa Moi. Sasa hivi hili linawezekana. Kumponda Rais sio ishu.
Hata hivyo baada ya umaarufu wa Fabish kuzidi kutokana na mageuzi aliyokuwa akiyafanya katika timu, taratibu mabango ya maandishi kama hayo yalianza kuonekana uwanjani licha ya Moi kuwa bado madarakani. Enzi za Fabish, viwanja vingejaa mashabiki kuja kutizama mechi. Kwa sasa hii imebaki stori.
Fabisch hakuwa kocha wa mchezo mchezo, alifanya mazoea ya kuletana juu na uongozi wa soka na hata mashabiki wenyewe kila alipohisi wanamzengua katika utekelezaji wa kazi yake.
Wakati moja alipozomewa na mashabiki baada ya Stars kuanza kufanya vibaya, Fabish aliwajibu kwa ujeuri kwa kuwaambia kwamba, ikiwa wanahisi hafanyi vizuri basi wamwajiri Yesu Kristo kuwa kocha sababu ni yeye tu ndiye asiyefanya makosa. Kauli hii ilimfanya kufutwa kazi mara mbili.
Alikuwa ni kocha mwenye utata, aliyejiamini na ambaye hakika kazi alikuwa akipiga si mchezo.
Ubishi wake  pamoja na drama zake ndizo zilizojaza mashabiki uwanjani. Fabicsh alitua kipindi, timu nyingi kama vile Abaluhya FC (AFC leopards), Luo Reunion (Gor Mahia) zilikuwa zimeanza kufifia hii ikiwa ni baada ya Rais Moi kutangaza kwamba timu zote zenye majina ya kikabila na kimaenzo  lazima zibadilishe majina au ndio zisambaratishwe kabisa.
Soka la kitaifa nalo lilikuwa likididimia. Wakati akipewa kazi 1987 Kenya ilikuwa ikishiriki mashindano ya Olimpiki, ambako aliishia kutia aibu huku kichapo cha magoli 7-1 walichopokezwa na Misri, ikisalia kuwa rekodi mbovu zaidi ya Stars
Ingawaje Fabicsh hakufanikiwa kuileta taifa mataji, soka la kitaifa liliamka katika kipindi chake  cha pili  alipoteuliwa kama kocha  baada ya kutimuliwa hapo awali.
Awamu hiyo ya pili kama kocha wa Stars ilianza 1997 . Aliigeuza timu na kuifanya wembe. Uwanja wa kitaifa wa Kasarani ukageuka kichinjio kwa timu nyingi zilizozuru kuchuana na Stars. Hiki ndicho kipindi mabango ya ‘Fabisch For President’ yalipata maarufu sana uwanjani.
Kipindi hiki cha awamu yake ya pili kama kocha, Fabisch aliitwa wakati Stars ilikuwa ikihangaikia matokeo ikishindwa kufanya vyema kwenye mechi za kufuzu kwa kombe la dunia 1998 na vile vile dimba la Bara Afrika. Fabicsh alifanikiwa kusuka kikosi  kilichofika mbali ikiwemo kutoka sare ya 1-1 na miamba wa Afrika kipindi hicho Super Eagles , Nigeria. Alifuatisha sare hiyo na Nigeria na  matokeo mengine mazuri kwa kuzishinda  Gabon na Guinea. ‘Fabisch For President’ ikawa ndio kauli mbiu ya mashabiki wengi. Kikosi alichokisuka kipindi hiki kiliibua  majina ya wakongwe wa soka kama vile John Baresi, Tom Ogweno, Eric ‘Cantona’ Ochieng, Ken Simiyu, John Lichuku, Wilberforce Mulamba, Micke Weche, na Bobby Ogolla.

AFUTWA TENA
 Muda mfupi baadaye alifutwa kazi tena na Shirikisho la soka wakati huo KFF (Kenya Football Federation) likisema Fabish alikuwa mjeuri sana. Kocha huyo naye  alijitetea kwa kusema Shirikisho halikuwa likimpa sapoti ya kutosha lakini hata zaidi lilifanya mazoea ya kumcheleweshea mshahara wake.
Akitimuliwa kwa mara ya pili, Stars walikuwa wamekuwa timu tishio katika ukanda huu wa Afrika Mashariki. Kazi yake ilipewa kocha Christian Chukwu ambaye alishusha tena kiwango cha Stars na kuilazimu KFF kumfuata Fabisch kwa mara ya tatu, waliyemrejesha kazini 2001 kipindi Kenya ikijiandaa kwa dimba la Cecafa. Kwa mara nyingine tena Fabisch aling’aa akiifikisha Stars fainalini al
ikopoteza dhidi ya Ethiopia.

AMWEKA OLIECH KWENYE MAP
Ni kipindi hiki cha awamu ya tatu uongozini mwaka 2002 ambapo  Fabisch alitambua kipaji kipya, straikaDennis Oliech. Kipindi hicho Oliech ambaye ndiye mfungaji bora wa yakati zote wa Stars, alikuwa na umri wa miaka 19 pekee. Fabish alianza kumpa namba kwenye kikosi chake cha kwanza pale Stars na kuchangia pakubwa nyota yake kung’aa kitaaluma.

Jhadi
Hadi anafariki dunia kazi yake ya mwisho ilikuwa ni kocha wa timu ya taifa ya Benin.  kansa. Hata hivyo sifa zake zinakumbukwa zaidi alipoifunza Zimbabwe(1992-95) na Harambee Stars.